Abiria mmoja amedaiwa kumkojolea
msafiri mwenzake, na kusababisha kuibuka kwa ngumi wakati ndege ya
Meditarranee ikiwa angani, vyombo vya Ufaransa vimesema.
Ndege hiyo ilikuwa angani kutokea
Jiji la Algiers nchini Algeria kwenda Ufaransa wakati ugomvi huo
ulipoibuka angani majira ya mchana na kulazimika kutua Lyon.
Abiria wameelezea tukio kuwa
lilikuwa ni la kushtua wakati mwanaume asiyenashati aliyedaiwa
kumkojolea abiria mwenzake akidhiditiwa na wahudumu wa ndege.
Imeelezwa kuwa abiria huyo alifanya
kitendo hicho kutokana na kupandwa na hasira kutokana na kutokunywa
kileo ama kuvuta sigara angani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni