UN
Clubs Tanzania Network kanda ya Dar es Salaam wakishirikiana na Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako wametoa msaada kwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha
Kurasini kwenye siku ya wapendanao ili kuonesha upendo mkubwa kwa
watoto hao. Vijana hao wa UN Club Tanzania Network wanafanya kazi siku
ya wapendanao nchi nzima za kusaidia jamii na vijana wa jijini Dar es
salaam wameungana na watoto wa kituo cha Kurasini kwa kutoa msaada na
wanafunzi hao wametoka katika shule za sekondari za Zanaki, Azania,
Benjamin na Jangwani.
Akizungumzia
msaada huo, Afisa Ustawi wa Jamii katika kituo hicho. Jack Omary
aliwashukuru kwa kuwatembelea siku ya wapendanao maana kuna watu wengine
wanaitumia siku ya wapendanao kwenye starehe na hata kutumia pesa bila
kuangalia kuna watu wanahitaji msaada. Nae Stella kutoka UN Clubs
Tanzania amesema lengo la kuja katika kituo cha watoto yatima cha
Kurasini nikujumuika na hao watoto ambao hawana wazazi na pia watoto
wenye shida mbalimbali.
Alisema inabidi kuwakumbuka hasa kwenye siku kama za wapendanao kwani kuna watu wanatumia pesa nyingi kwenye starehe kuliko kutoa misaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu hasa wazee,walemavu na hata watoto yatima. Mtoto Aboubakary Seif anayelelewa katika kituo hicho cha Kurasini amewashukuru UN Clubs Tanzania Network Pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako kwa kuwaona kama watu katika jamii wanakubalika hasa kwenye siku ya wapendanao.
Amesema wao wamesijsikia furaha kutembelewa na vijana wenzao na kuwapa moyo hasa kwa kusoma kwa bidii ili kufikia malengo waliyojiwekea. Pia aliwaomba watu wengine wenye uwezo waje kutoa msaada maana matatizo ni mengi na matatizo hayo yatatatuliwa kwa misaada ya wadau mbalimbali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni