Makamu
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani
akizungumza katika mkutano wa wadau kujadili maendeleo ya tafiti, elimu,
matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini katika kipindi
cha miaka 10 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Profesa Makani pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Sikoseli ni
ugonjwa wa kurithi kutoka kwa wazazi wenye vinasaba vya ugonjwa huo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.
Mpoki Ulisubisya (kulia) akizungumza na baadhi ya wadau walioshiriki
mkutano kujadili maendeleo ya tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu
ugonjwa wa sikoseli nchini katika kipindi cha miaka 10 katika hafla
iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa
Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani ambaye pia ni
Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Makamu
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani
(wa pili kushoto), ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya
Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
akiwa na baadhi ya wadau walihudhuria mkutano kujadili maendeleo ya
tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini
katika kipindi cha miaka 10 jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto
ni, Prof. Japhet Killewo, mhadhiri kutoka MUHAS, Dk, Namala Mkopi,
daktari bingwa wa watoto na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa
Watoto (PAT) na Promise Mwakale, Ofisa Uhusiano katika taasisi ya
sikoseli.
Mratibu
wa matibabu ya Sikoseli katika kitengo ugonjwa huo kwenye Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Deogratius Soka (katikati) akibadilishana
mawazo na wadau. Kushoto ni Promise Mwakale, Ofisa Uhusiano katika
taasisi ya sikoseli na kulia ni Dk, Namala Mkopi, daktari bingwa wa
watoto na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Watoto (PAT).
Imeelezwa Tanzania ni moja ya nchi yenye inadadi kubwa ya wagonjwa wa
sikoseli ikikadiriwa kuwa watoto kati ya 8,000 na 11,000 huzaliwa kila
mwaka wakiwa tatizo hilo.
Mmoja
wa watu wanaosumbuliwa na tatizo la sikoseli, Hadija Abdallah (20)
akitoa ushuhuda wake jinsi anavyoweza kuishi maisha ya kawaida licha ya
kugunduliwa na ugonjwa huo akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu.
Makamu
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani
(wa pili kushoto), ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya
Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
akiwa na baadhi ya wadau walihudhuria mkutano kujadili maendeleo ya
tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini
katika kipindi cha miaka 10 jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Dk. Neema Rusibimayila na Dk Sarah
Maongezi mkurugenzi masuala ya afya wa Mfuko wa Wanawake na Maendeleo
(WAMA).
Ofisa
Mtendaji wa Mkuu wa Benjamin William Mkapa Hiv/Aids Foundation, Hellen
Mkondya-Senkoro (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Deloitte, Zahra
Nensi huku Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT),
Prof. Julie Makani akiangalia wakati wa hafla hiyo. Imeelezwa ugonjwa
wa sikoseli unatibika kirahisi endapo utagundulika mapema katika umri
mdogo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni