Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa
Kakukuru,Ukerewe ikiwa siku ya mwisho ya ziara yake mkoani Mwanza.
Katibu
Mkuu amekamilisha ziara ya kutembelea majimbo yote ya Uchaguzi nchi
nzima ambapo amejionea utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi unavyooendelea
pamoja na uhai wa Chama Cha Mapinduzi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Magessa Mulongo akihutubia wakazi wa Kakukuru wilayani Ukerewe.
Wakazi
wa Kakukuru ,Ukerewe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman
Kinana kabla ya kuzindua shina la wakereketwa wa CCM Kakukuru.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya Chama
wakati wa uzinduzi wa shina la wakereketwa Kakukuru wilayani Ukerewe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya maendeleo ya
mradi wa maji Kazilankanda uliopo kijiji cha Chabilungo ,Ukerewe
utakaonufaisha vijiji 13 kutoka kwa msimamizi wa mradi Revocatus
Migarambo .
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ukerewe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ukerewe ambapo aliwaambia wana CCM
wasikae kimya badala yake waseme yale mambo ya wapinzani ambayo hayapo
sawa, akitolea mfano halmashauri ya Ukerewe ipo chini ya upinzani na
hakuna kinachofanyika hivyo si vyema kukalia jambo hilo ni vyema
wananchi wafahamu .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Nansio
katika Uwanja cha Mongella ambapo aliwaambia wananchi hao
wasichagueviongozi kishabiki kwani ushabiki unaweza wachelewesha sana
kimaendeleo,alitoa mfano halmashauri ya wilaya ya Ukerewe ipo upinzani
na hakuna jambo la maendeleo linafanyika mpaka sasa.
Bibi akisikiliza mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa Mongella ,Nansio wilaya ya Ukerewe.
Katibu Mkuu na ujumbe wake wakiondoka eneo la mkutano Nansio kwa mguu kwenda kupanda meli tayari kwa kurudi Mwanza mjini
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliokuja kumpokea akitokea Ukerewe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni