Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu akizungumza na akinamama wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM
(UWT) na kuwaomba kushirikiana na kuhakikisha wanashinda na kupata
heshima hiyo. Baadhi
ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na
mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi.
Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM
Dodoma. Mgombea

heshima hiyo. Mgombea

Dodoma.[/caption]
MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Bi. Samia Suluhu amefanya mazungumzo na wanachama wa Umoja wa Wanawake
wa CCM (UWT) na kuwaomba kuitumia vema heshima na nafasi waliopewa
akinamama nchini ya kushika nafasi ya makamu wa rais kwa mara ya kwanza,
hivyo kuhakikisha wanahamasisha wenzao ili CCM iweze kushinda na
wanawake kutwaa heshima hiyo.
Bi. Suluhu amesema hayo alipokuwa akizungumza na akinamama wa UWT mkoani
Dodoma ikiwa pamoja na kutaja kipaumbele ambapo kimewekwa kwa akinamama
katika ilani mpya ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25,
2015. Alisema atatumia nafasi yake kushawishi akinamama kipata vifaa na
mazingira rafiki ya kuendesha kilimo cha kisasa ili waweze kukuza uchumi
wao, pia kuwawezesha katika vikundi vya ujasiliamali ikiwa ni pamoja na
kukomesha usumbufu ambao akinamama wafanyabiashara wamekuwa
wakibughuziwa na mgambo wa jiji.
Mgombea huyo alisema kupitia vikundi akinamama watawezeshwa na fungu la
fedha shilingi milioni hamsini fedha ambazo zitatolewa kila kijiji
maalumu kwa ajili ya kuwawezesha akinamama pamoja na vijana ili waweze
kukuza mitaji yao. Pamoja na hayo Bi. Suluhu alisema Serikali
watakayoiunda itashughulikiwa changamoto anuai wanazokumbana nazo
walemavu hasa akinamama ili kuwawezesha na wao katika ushindani. "...Kwa
upande wa kilimo nitahakikisha nachochea kidogo kidogo ili wanawake
wapate vitu kama pembejeo na vifaa vingine kuwawezesha kuendesha kilimo
cha kisasa," alisema. Mmoja
wa wajumbe wa kamati ya taifa ya kampeni za CCM, Bi. Ummy Mwalimu
akitoa neno katika mkutano na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM
(UWT) kwenye Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taifa ya kampeni za CCM (mbele)
walioambatana na mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu wakiwa katika mkutano
na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) katika Ukumbi wa NEC
ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma. Mke
wa waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda akizungumza na wanachama wa
Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kabla ya mkutano huo na mgombea mwenza
wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana
kuanza katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma. Mmoja
wa wajumbe wa kamati ya taifa ya kampeni za CCM, Bi. Asumpta Mshama
akitoa neno katika mkutano na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM
(UWT) kwenye Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma. Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) mkoani Dodoma, Bi. Salome Kiwaya
akizungumza kabla ya mkutano huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana kuanza katika Ukumbi
wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma. Baadhi
ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na
mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi.
Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM
Dodoma. Baadhi
ya wawakilishi wa makundi anuai katika wanachama wa Umoja wa Wanawake
wa CCM (UWT) wakitoa neno kuwawakilisha wajumbe wenzao katika mkutano
huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM
Dodoma. Makundi ambalimbali
ya akinamama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) mkoani Dodoma, wakimpa
zawadi mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika
Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.
Alisema
ilani ya CCM imetoa kipaumbele kwa huduma za afya hasa huduma za mama
na mtoto ikiwa ni kutambua changamoto na matatizo wanayokumbana nayo
akinamama eneo hilo. Alisema atadhibiti rushwa na matumizi mabaya ya
dawa zinazopelekwa wizara ya afya kuhakikisha zinafanya kazi kama
ilivyokusudiwa na kudhibiti urasimu.
Aliongeza
kuwa baada ya ujenzi wa shule za kata kufanikiwa akiingia madarakani
anaongeza nguvu katika ujenzi wa mabweni ya wasichana ili kukabiliana na
changamoto ya mimba kwa wanafunzi wasichana ambazo zimekuwa
zikichangiwa na wao kutembea umbali mrefu na kupata changamoto njiani.
Aidha aliongeza kuwa ili kuonesha Serikali ya CCM inawajali walimu
itaunda chombo maalumu ambacho kitakuwa na kazi ya kushughulikia
matatizo ya walimu pamoja na kukiwezesha kuhakikisha kinatimiza majukumu
yake kiufasaha.
Aliwaomba akinamama kushirikiana kufanya kampeni na kuhakikisha CCM
inashinda hivyo akinamama kupata fursa hiyo waliyopewa na CCM kwa sasa.
"...Naombeni tushirikiane wote kufanya kampeni nyumba kwa nyumba,
kitanda kwa kitanda na shuka kwa shuka ili kuhakikisha tunashinda maana
hii ni zawadi kwa akinamama tujitahidi tuweze kushinda nafasi hii,"
alisema Bi. Suluhu. Baadhi
ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na
mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi.
Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM
Dodoma. Baadhi
ya wawakilishi wa makundi anuai katika wanachama wa Umoja wa Wanawake
wa CCM (UWT) wakitoa neno kuwawakilisha wajumbe wenzao katika mkutano
huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM
Dodoma.
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika
mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu
ya CCM Dodoma.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni