Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, Sundi Samike,
akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane
chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni zilizotolewa na MO Dewji
Foundation (shilingi 14 milioni) na Doris Mollel Foundation shilingi 2.3
milioni).
Mwakilishi
wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane shule ya msingi
Kibaoni mjini Singida, chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16.
Duda amewataka wakazi wa manispaa ya Singida, kujenga utamaduni wa
kuchangia kwa hali na mali, uboreshaji wa mazingira ya shule, ili
kuvutia wanafunzi kupenda shule.
Mkurugenzi
wa Doris Mollel Foundation ya jijini Dar-es-sa-laam, Doris Mollel,
akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane ya
shule ya msingi Kibaoni mjini Singida chenye thamani ya zaidi ya
shilingi 16 milioni, kati ya fedha hizo, Mo Dewji Foundation imetoa
shilingi 14 milioni na Doris Foundation shilingi 2.3 milioni.
Mwakilishi
wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa tatu kulia)
akiteta jambo na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel (wa
pili kulia) wakielekea kuzindua choo bora kipya cha shule ya msingi
Kibaoni.
Mwakilishi
wa MO Dewji mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa pili kushoto) na
Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundatin, Doris Mollel (wa tatu kushoto) kwa
pamoja wakizindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni chenye
thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni. MO Dweji Foundation imechangia
shilingi 14 milioni na Doris Mollel, shilingi 2.3 milioni.
Jengo
la choo bora chenye matundu nane kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya
shilingi 16 milioni kwa ushirikiano wa MO Dewji Foundation na Doris
Mollel Foundation kitakachotumiwa na wanafunzi 842 wa shule ya msingi
Kibaoni mjini Singida. (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
WAZAZI/WALEZI
wakazi wa halmashauri ya manispaa ya Singida, wamehimizwa kujenga
utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali uboreshaji wa mazingira ya
shule, kama njia moja wapo ya kuwavutia wanafunzi kuhudhuria shule.
Wito
huo umetolewa na Mwakilishi wa MO Dewji Foundation mkoa wa Singida,
Duda Mughenyi, wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora
chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa
shule ya msingi Kibaoni mjini hapa, yenye jumla ya wanafunzi 842, kati
yao wavulana ni 377 na wasichana ni 465.
Alisema
uzoefu unaonyesha kwamba mazingira ya shule yakiwa safi, vifaa vya
kufundishia na kujifunzia viwepo vya kutosha , maji safi na salama
yawepo na vyoo bora vinavyokidhi mahitaji, hatua hiyo huwajengea
mazingira mazuri wanafunzi , kujiendeleza kielimu.
Akifafanua,
alisema shule ya msingi ya Kibaoni ilikaribia kufungwa kutokana na
kukosa vyoo kwa ajili ya wanafunzi na wanafunzi,lakini Dewji Foundation
na Doris Mollel Foundation, ilinusuru shule hiyo isifungwe baada ya MO
Dewji Foundation kutoa shilingi 14 milioni na Doris Mollel kutoa
shilingi 2,300,000.
Duda alitumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi wakitunze na kudumisha usafi wa choo hicho ili kiweze kutumika kwa muda mrefu.
Kwa
upande wake Doris Mollel (Miss Singida 2014), alisema Foundation yake
itaendelea kufadhili sekta ya elimu mkoani Singida kama njia ya
kuwashukuru wakazi mkoani hapa kwa kumsapoti na kufanikisha kushinda
nafasi ya Miss Singida mwaka jana.
Awali
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kindai tarafa ya Mungumaji
iliyoanzishwa mwaka 1975,Sundi Samike,alishukuru uongozi wa Mo Dweji
Foundation na Doris Mollel Foundation, kwa kuifadhili shule hiyo ujenzi
wa choo na kuinusuru kufungiwa.
“Nitumie
nafasi hii pia kulipongeza shirika la WaterAid Tanzania kwa uamuzi wake
wa kufadhili ujenzi wa vyoo bora ambao ujenzi wake tayari
umeishaanza.Aidha,nitoe wito kwa wazazi,wasaidie kwa hali na mali
kuharakisha ujenzi huu”,alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni