Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vothanh Nam naye akizungumza katika hafla hiyo |
Afisa Mambo ya Nje Bw. Emmanuel Luangisa (katikati) akifuatilia hotuba kwenye kitabu iliyokuwa ikisomwa na Mhe. Waziri Mkuu (hayupo pichani) |
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Vothanh Nam (kushoto) wakitakiana afya njema kwenye hafla hiyo. |
Mhe. Pinda akikata Keki pamoja na Balozi Nam ikiwa ni ishara ya kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam. |
Balozi wa Vietnam, Mhe. Nam (kulia) akimpokea Waziri Mkuu, Mhe. Pinda (kushoto) alipowasili kwenye maadhimisho hayo anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Yahya Simba |
Mhe. Pinda (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga. |
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda akisalimiana na raia wa Vietnam waishio nchini waliojitokeza kumpokea alipowasili kwenye maadhimisho hayo. |
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vothanh Nam (kushoto) wakiwa wamesimama kwa pamoja tayari kwa nyimbo za mataifa yao. |
Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini nao wakiwa wamesimama tayari kwa kuimba nyimbo za Taifa |
Kikundi cha Polisi cha Brass Band kikipiga nyimbo za Mataifa hayo mawili wakati wa Maadhimisho hayo |
Sehemu ya wageni waalikwa kwenye maadhimisho hayo. |
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nao wakiwa na nyuso za furaha wakati wa maadhimisho hayo.
Picha na Reginald Philip
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni