Mtuhumiwa
mauaji ya kutisha ya kumkata viungo vya mwili marehemu zikiwemo sehemu
za siri, viganja vya mikono na matiti mauaji yaliotokea kwenye hoteli ya
A Square Belmot amekamatwa na jeshi la polisi mkoani Arusha.
Akiongea
na vyombo vya habari ofisini kwake kamanda wa polisi, Naibu kamishna wa
jeshi la polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alisema kuwa mtuhumiwa
alikamatwa juzi majira ya asubuhi katika eneo la TRA House jijini
Arusha.
Sabas
alisema kuwa alipohojiwa na polisi alikiri kushiriki mauaji hayo na
ndipo alipowapeleka kuwaonyesha polisi alipovitupa viungo vya marehemu
eneo la mto misheni usa river nje wilayani meru.
Alisema
kuwa marehemu ametambuliwa jina kamili Alfred Kimbaa mwenye umri wa
miaka18 mkazi wa mianzini jijini hapa huku mtuhumiwa ambaye jina lake
limetambuliwa kwa Elijus Lyatuu mkazi wa Dar es Salaam ambaye marehemu
alikuwa akiuza duka la kaka yake alietambuliwa kwa jina moja la Lyatuu
anaeishi jijini Dar es salaam.
Alisema
kuwa mtuhumiwa ni mwanafunzi wa mwaka wa tano chuo cha falsafa cha
kanisa katoliki Segerea na alipofika Arusha kwa mara ya kwanza aliishi
na marehemu chumba kimoja kabla ya mgogoro kuanza na ndipo alipofikia
kumuua marehemu na kuiacha maiti yake katika hotel nae kutokomea
kusikojulikana hadi alipokamatwa juzi.
Alisema
kuwa mtuhumiwa Elijus alimua marehemu kwanza kabla ya kuanza kucharanga
viungo ndio maana chumbani alikokutwa marehemu hakukua na damu.
“Tukio
hili lisihusishwe na imani za kishirikina kwani kulikuwa na mgogoro
kati ya mtuhumiwa na marehemu uliopelekea mtuhumiwa kufanya tukio
hilo”alisema Kamanda Sabas
Upelelezi ukikamilika na taratibu za jeshi la polisi zinaendelea na zikikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni