RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA PAMOJA NA KUFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KATIKA WODI YA WAZAZI YA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir ambaye amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akimuombea Dua Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kumjulia hali Hospitalini hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa Dua na ndugu na jamaa mbalimbali ambao walifika Muhimbili kuwaona wagonjwa wao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea katika Wodi ya Wazazi kufanya ukaguzi wa ghafla mara baada ya kuwasili akitokea Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya Wazazi na amewahidi kutatua kero zao ndani ya muda mfupi ujao.PICHA NA IKULU

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni