Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi Dr Sr Hellen Bandiho akifungua rasmi kusanyiko la mahafali.
Dk Hamis Mwinimvua katikati
aliyemuwakilisha Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa Bodi, Dk Sr Hellen Bandiho na Mtendaji Mkuu Clemence Tesha wakimshuhudia
Mgeni Rasmi akizidua mtaala mpya.
Dk Hamis Mwinimvua
akitoa hutuba kwa niaba ya mgeni rasmi.
Mgeni
Rasmi, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na baadhi ya wahitimu katika picha ya
pamoja
Sehemu ya
wahitimu wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
WATAALAM wa Ununuzi na
Ugavi nchini wameaswa kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia miiko na
maadili inayoongoza taaluma yao ili kuleta tija kwenye matumizi ya fedha za
watanzania. Aidha Bodi imeagizwa kusimamia kwa ukaribu zaidi mienendo ya
wanataaluma waliosajiliwa.
Hayo yalisemwa na Dk. Hamis Mwinimvua Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha akimwakilisha Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha Mheshimiwa Saada Mkuya Salum kwenye sherehe
za mahafali ya sita ya wataalam wa ununuzi na ugavi (PSPTB).
Aidha Bodi imepongezwa kwa
kuzindua mtaala mpya wa masomo utakaonza kufundishwa kuanzia Januari 2016 na
kutahiniwa mwezi Novemba 2016. “ni matumaini yangu pia kuwa mtaala huo
utawajengea uwezo wataalam wote wa ununuzi na ugavi ili wazidi kuwa mahiri na
wenye weledi mkubwa katika kufanya kazi zao” alisisitiza.
Waziri wa Fedha aliipongeza Bodi
kwa kuongeza masomo ya maadili,
ujasiliamali, utafutaji wa masoko na usimamizi wa mikataba kwani eneo hili ni mahsusi katika kuleta maendeleo na tija katika
matumizi ya rasilimali fedha. “ni matumaini yangu kwamba masomo haya yatakuza
ajira kwani yatafungua wigo kwa wahitimu kuanza kujiajiri” alisema Mheshimiwa
Waziri. Pia aliongeza kusema, serikali kwa upande wake imeboresha na itaendelea
kuboresha zaidi mazingira ya ajira binafsi kwa minajili ya kuwawezesha wananchi
kujipatia kipato halali cha kuendesha maisha yao.
Aidha aliwaagiza waajiri wote kuhakikisha kwamba wanazingatia mahitaji ya sheria
juzuu Na 179, inayowataka kuhakikisha kwamba wanaajiri watumishi waliosajiliwa
na Bodi.
Alihitimisha kwa
kuwapongeza wahitimu 494 walitunukukiwa vyeti katika ngazi za cheti cha awali,
msingi na taaluma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni