Hapa
ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambako wanawake/akina mama
zaidi ya 300 wa manispaa ya Shinyanga wamekutana kujadili namna ya
kupambana na ugonjwa wa Kipindupindu ambao umeukumba mkoa wa
Shinyanga.Mkutano huo umeitishwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro.Akina mama hao waliojitokeza kwa wingi leo jioni Oktoba
06,2015 wameweka mikakati mbalimbali ya kutokemeza ugonjwa kipindupindu
ambapo Jana pekee wagonjwa 9 wamelazwa katika kambi maalum jirani na
hospital ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambapo kati ya hao 9 wawili
wamefariki dunia.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa mkutano
wake na wanawake zaidi ya 300 katika manispaa ya Shinyanga uliofanyika
katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine
alisema wanawake ni jeshi kubwa na ni walimu wakubwa katika familia
hivyo wana nafasi kubwa ya kupambana na kipindu pindu kwa kuimarisha na
kuhamasisha usafi kwa akina baba,watoto na hata wanawake wenzao.
"Kipindu
pindu ni hatari sana...kinaua lazima tupambane nao kwa nguvu
zote..nimewaita ili kila mmoja ajue Shinyanga tuna janga..sasa kila mtu
achukue hatua,ugonjwa huu unatokana na uchafu..akina mama mna nafasi
kubwa sana katika hili...."alisema Matiro.
Akina mama wakiwa wamenyoosha mikono...kwamba wako tayari kupambana na kipindupindu.....
Mkuu
huyo wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwaeleza akina mama hao
kuwa chanzo cha ugonjwa huo ni uchafu yaani kula au kunywa kinyesi cha
mtu mwingine hivyo ili kuhakikisha ugonjwa kipindu pindu ni vyema
wananchi wakajenga vyoo,kuepuka kunywa maji yasiyochemshwa,kula vyakula
vya moto,kuosha matunda kabla ya kula sambamba na kuepuka kunywa pombe
za kienyeji.
Afisa
afya mkuu wa manispaa ya Shinyanga Elly Nakuzelwa akizungumza wakati wa
mkutano huo ambapo alisema ugonjwa huo unazidi kuenea kwa kasi katika
manispaa ya Shinyanga ambapo jana pekee wagonjwa 9 walifikishwa katika
kambi maalum ya wagonjwa wa kipindu pindu jirani na hospitali ya rufaa
ya mkoa wa Shinyanga.
Afisa
afya huyo alisema ili kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa katika
manispaa ya Shinyanga tayari wamepiga marufuku tabia ya akina mama lishe
na baba lishe kutembeza vyakula mtaani,unywaji pombe za kienyeji,kuzuia
matanga kwenye familia yoyote iliyopatwa na kifo pamoja na kula vyakula
kwenye sherehe yoyote.
Afisa
afya mkuu wa manispaa ya Shinyanga Elly Nakuzelwa aliwataka wakazi wa
Shinyanga kufika haraka hospitali pindi wanapoona dalili za ugonjwa wa
kipindupindu ikiwemo kuharisha na kutapika mfululizo.
Mkutano unaendelea
Nakuzelwa
aliwataka wananchi kujenga tabia ya kufunika vyoo vya shimo,kuepuka
kula vyakula kwenye mikusanyiko ya watu wengi,kuacha kutembeza vyakula
mtaani,kuuza vyakula shuleni,kununua mboga zinazouzwa chini badala ya
kwenye meza.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza juu ya matumizi ya
vyoo majumbani kwani chanzo kikubwa cha ugonjwa wa kipindupindu ni
kunywa au kula kinyesi cha mtu mwingine baada ya kuchanganyikana na
vyakula ama maji anayokunywa binadamu.
Akina
mama kutoka manispaa ya Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
ukumbini ambapo walikubaliana kuimarisha usafi ili kutokomeza ugonjwa
hatari wa kipindupindu
Miongoni mwa dalili za ugonjwa wa kipindu pindu zilizotajwa ukumbini ni pamoja na kuharisha na kutapika mfululizo.
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Akina mama wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Viongozi
mbalimbali wa mitaa katika manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano
wa akina mama katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga
Mmoja wa akina mama hao akichangia mawili matatu katika mkutano huo
Katika
mkutano huo pia ilibainika kuwa wananchi wengi mjini Shinyanga hawana
vyoo hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kuenea kwa ugonjwa wa
kipindupindu
Wanawake hao pia walisisitizwa kujenga tabia ya kuwaelimisha wanaume juu ya umuhimu wa kujenga vyoo
Mkutano unaendelea
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumzia kuhusu amani ya
nchi ambapo alisema serikali imejipanga vyema kukabiliana na watu
waliojiandaa kufanya vurugu ikiwemo kuzuia wanawake na wazee wasipige
kura siku ya uchaguzi mkuu nchini utakaofanyika Oktoba 25,2015.
Wanawake
hao pia walihamasishana kushiriki uchaguzi mkuu ujao huku wakiiomba
serikali kuimarisha ulinzi kwao na wazee kwani kumezuka uvumi kuwa kuna
watu watawazuia kushiriki uchaguzi Oktoba 25 mwaka huu
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akawahamasisha wanawake
kushiriki katika shughuli za maendeleo badala ya kutegemea
wanaume...akasisitiza juu ya umuhimu wa kujiunga katika vikundi vya
wajasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia kwa urahisi zaidi badala ya
kufuata mtu mmoja mmoja
Akina mama wakisikiliza kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Maendeleo bila amani ni kazi bure...akina mama wakahamasishana kushiriki kulinda amani ya nchi....
Hakuna
kutishana siku ya uchaguzi...mkuu wa wilaya ya Shinyanga
akawahakikishia ulinzi siku ya uchaguzi huku akiwataka kulinda kadi zao
za kupigia kura.
Wanawake na maendeleo ndiyo makubaliano waliyoafikiana.....
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Afisa mtendaji kata ya Shinyanga Mjini Mathias Masalu akizungumza katika mkutano huo
Mwenyekiti wa mtaa wa Kaunda Joha Mussa akifunga mkutano huo
Akina mama wakitawanyika baada ya mkutano
Kila mmoja na njia yake...kushoto ni Mama Steve na Marietha William wakirudi kwao
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni