Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na
Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini, Al Amin Yusuph, akizungumza katika kongamano lililowakutanisha
watendaji kutoka Redio za jamii nchini katika mji wa Terat, wilayani
Simanjiro mkoa wa Manyara jana.
Mwenyekiti wa Muungano wa Redio za
Kijamii nchini (COMNETA), Sekiku Joseph akizungumza katika Kongamano
hilo ambalo amesisitiza umuhimu wa viongozi wa Radio za kijamii
kuthamini michango inayotolewa na wafadhili ili iweze kuwa endelevu.
Mshauri na Mkufunzi wa masuala ya
vyombo vya habari jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akisistiza jambo
katika mafunzo hayo.
Afisa Miradi mpya wa Unesco, Nancy Kaizirege akisisitiza jambo.
Mkurugenzi wa Redio ya Jamii Uvinza FM,
Ayub Kalufya akichangia mada na kuomba Unesco kuendelea kutoa usaidizi
kwao kutokana na mchango wanaoutoa kwa jamii.
Afisa Miradi mpya wa Unesco, Nancy
Kaizirege akisisitiza jambo wakati mafunzo hayo yakiendelea. kulia ni
Meneja wa Orkonerei Radio Service Simanjiro Manyara (ORS FM), Bw.Baraka
Ole Maika.
Mwenyekiti wa Bodi ya Redio ya Jamii
94.9 FM , Mkoani Pemba, Hamidu Hassan Bakari akizungumza namna Redio
yake itakavyonufaika kupitia mafunzo ya kuwajengea uwezo na vifaa ya
matangazo.
Meneja wa Redio Kahama FM, Marco Mipawa, akizungumza jambo.
Mwandishi Wetu,Simanjiro
Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO) limeendelea kuimarisha Redio za Jamii
nchini kwa kuwapa mafunzo ya mara kwa mara watendaji wa ngazi
mbalimbali kwa lengo la kuzifanya Redio hizo kuwahudumia vema wananchi
wanaoishi maeneo ya vijijini.
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na
Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini, Al Amin Yusuph amesema kumekuwa na mafanikio tangu mradi huo
kuanza miaka mitatu iliyopita chini ya ufadhili wa UNESCO, Shirika la
Maendeleo la Sweden (SIDA) na Serikali ya Uswizi ambapo licha ya
kuwajengea uwezo vifaa vya kieletroniki vilitolewa kwa Redio hizo.
Kongamano hilo la mwaka la siku tatu(3)
linafanyika katika Kituo cha Orkonerei Radio Service Simanjiro Manyara
(ORS), Terat wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara na limewaleta pamoja
watendaji wa Redio za Jamii 20 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara
na Zanzibar .
“Tunalenga kuwajengea uwezo ili hizi
Redio za Jamii zifanye kazi kwa weredi ya kuleta maendeleo endelevu kwa
wananchi waweze kushiriki mijadala inayohusu sekta za afya, elimu na
kilimo,”amesema Yusuph
UNESCO inafanya kazi kwa karibu na Muungano wa Radio za Kijamii Tanzania(COMNETA)unaongozwa na Mwenyekiti wake Sekiku Joseph.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni