Mkurugenzi
Idara ya Habari, Assah Mwambene (kulia) akionesha kitabu cha Katiba ya
Tanzania kifungu kinachompa mamlaka Rais kufanya uteuzi ilikuboresha
Serikali yake awapo madarakani. kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Vicent Tiganya. Mkutano huo umefanyika
leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam (Picha
zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Andrew Chale.
DAR
ES SALAAM Kufuatia vyombo vya habari nchini kuripoti taarifa kuhusiana
na uteuzi wa Rais wa Wakuu wapya wa Wilaya uliofanyika hivi k aribuni,
baadhi ya vyombo hivyo vya habari ikiwemo moja ya gazeti la kila siku
nchini kuripoti kuwa uteuzi huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya kulipa
fadhila na umetokana na masuala ya kisiasa na ni ufujaji wa wa fedha za
umma. Hata hivyo Serikali imetolea ufafanuzi wa suala hilo kupitia
Msemaji mkuu wa Serikali.
Akizungumza
na waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene amefafanua kuwa, Serikali
imetimiza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu na Rais
ana mamlaka ya kufanya uteuzi wakati wowote inapobidi kwa malengo ya
kuboresha utendaji kazi Serikalini hivyo utezi huo wa Wakuu wa Wilaya
ulizingatia vigezo vyote na taarifa hizo zilizoripotiwa na gazeti hilo
ni za uzushi na za kupuuzwa.
“Serikali
inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya
uliofanywa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete tarehe 4/10/2015 ambapo jumla ya Wakuu hao wapya wa
Wilaya 13 waliteuliwa na wengine Saba kuhamishwa vituo vua kazi.
Hii
ni kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu alizonazo Rais” alieleza
Assah Mwambene katika ufafanuzi wake kwa vyombo vya habari.
Na kuongeza kuwa, taarifa hizo zilizoripotiwa ni za kichochezi na zinalenga kumchonganisha Mhe.Rais na wananchi wake.
Mkurugenzi
ihuyo, aliongeza kuwa, Serikali inapenda kuvikumbusha vyombo vya habari
kufanya utafiti kwa kusoma nyaraka mbalimbali kuhusu mamlaka ya Rais na
kujiridhisha kama uteuzi huo umezingatia matakwa ya Katiba ya nchi au
la.
“Aidha,
tunaviomba vyombo vya habari kuandika habari zenye lengo la kujenga
umoja na mshikamano badala ya kuandika habari zenye lengo la kuwagawa
Watanzania.” Alimalizia Mkurugenzi huyo.
Mbali
na kutolea ufafanuzi huo juu ya taarifa za uzushi, pia aliwataka
wamiliki wa mitandao ya kijamii ikiwemo blog pamoja na wananchi
wanaotumia mitandao hiyo ya kijamii kuweka taarifa zisizo za kweli na
zinazopotosha umma, amewataka waache mara moja kwani Serikali
inazifanyia kazi taarifa zote na muda wowote watachukuliwa hatua.
“Kumekuwa
na taarifa za blog za habari kuweka habari za uongo na kuhaminisha watu
habari zao hizo bila kufuata misingi na kanuni. Wapo walioripoti habari
za uongo kwa kumsingizia kifo Waziri Abdala Kigoda kuwa amefariki
dunia… huo ni uzushi na tumeendelea kukanusha kwa hilo pia kuna mtu
alilipoti kuwa Mkuu wa Majeshi kunywesha sumu hilo nalo si la kweli huo
wote ni uzushi unaoenezwa na watu kupitia blog na baadhi ya vyombo vya
habari serikali itazichukulia sheria kali” amebainisha Mkurugenzi huyo.
Katika
mkutano huo Assah Mwambene ametumia muda huo kuwataka waandishi
kuzingatia wed=redi wa habari huku akiimiza kuchukua vitambulisho vya
Serikali’Press Card’ kwani ndio vyenye dhamana ya kuwatambua katika
weredi wao na utendaji makini katika kazi zao za kihabari.
“Mwandishi
unatakiwa uwe na Press Card. Hii ni kama unavyoona leseni ya kibiashara
kwa mfanyabiashara kuwa na leseni na mwandishi tunampatia leseni ambayo
ni press card ambayo ndio inamfanya afanye kazi zake kwa uhuru”
alimalizia Mkurugenzi huo.
Mkurugenzi Idara ya Habari, Assah Mwambene (kulia) akitoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari
muda wa maswali na majibu...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni