Na Beatrice Lyimo-Maelezo
SERIKALI
imesema itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake na Jamhuri ya Watu wa
China kwa kuimarisha fursa mbalimbali za kijamii ikiwemo nyanja ya kiutamaduni.
Hayo
yamesemwa leo Jumatatu (Oktoba 12, 2015)Jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene wakati wa halfa ya
uzinduzi wa chaneli mpya ya filamu ya China –Africa Movies
itakayoonyeshwa kupitia kituo cha televisheni cha Easy Television
kilichopo nchini.
Bw.
Mwambene amesema kuwa uwepo wa chaneli hiyo utasaidia wazalishaji wa
Tanzania kuonekana na kujulikana kimataifa na kuweza kujiongezea kipato
na fursa kwa waandaaji hao.
“Chaneli
hii itawapa fursa kwa pande zote mbili kwani filamu ya Tanzania
itaonyeshwa china na kutafsiriwa kwa lugha yao na kwa upande wa Tanzania
filamu za china zitaonyeshwa hapa Tanzania na kutafsiriwa kwa lugha ya
Kiswahili”
Aidha
Mwambene alisema Chaneli ya China –Africa movies, licha ya
kuwa daraja la kujifunza tamaduni za kichina pia itatoa fursa kwa
Watanzania kuweza kujifunza mbinu mbalimbali za biashara na kufungua
milango kwa Watanzania kufahamu hatua mbalimbali za maendeleo ya
kiuchumi na kiutamaduni.
Mwambene
ameitaka Idara ya filamu nchini China kuitembelea Wizara ya Habari,
Vijana, Michezo na Utamaduni kwani ina kitengo kinachohusika na filamu
za ndani.
Kwa
upande wake Waziri wa Radio, Televisheni na usimamizi wa filamu wa
Jimbo la Henan, China Bi. Song Fengxian alisema Serikali ya China
itaongeza ubunifu kwa watazamaji wa pande zote mbili na kuwashukuru
wadau wote waliosaidia kufanikisha uzinduzi wa filamu hiyo.
Naye
mwakilishi wa Kituo cha EASY TV Bi. Sophia Selis alisema kuwa katika
kuendeleza urafiki baina ya Tanzania na China, kituo cha Easy Television
imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha, kujifunza na kubadilishana
utamaduni kulingana na wakati.
“Tunarusha
program zetu kwa kutumia lugha mbalimbali ikiwemo kiingereza, kichina,
kiarabu, kihindi na Kiswahili ili kukidhi tija za watazamaji wetu wa
mataifa mbalimbali kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayotoa picha zenye
ubora” alisema Bi. Selis.
Easy
television inarusha jumla ya chaneli 33 vya televisheni ikiwemo filamu,
muziki, burudani, michezo, matukio, habari, vipindi vya watoto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni