
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula (kulia) pamoja
na mtendaji mkuu wa UTT-PID Dr. Gration Kamugisha (kushoto) wakiweka
sahihi mikataba ya makubaliano ya uendelezaji wa maeneo hayo
yanayomilikiwa na wizara katika balozi mbalimbali ili yawe na manufaa
kibiashara huku wakishuudiwa na wasaidizi wao.
Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wakishuhudia utiaji wa Sahihi katika mkataba wa Makubaliano hayo.
Wakibadilishana mikataba ya ushirikiano na makubaliano hayo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula (kulia)
wakipeana mikono na na mtendaji mkuu wa UTT-PID Dr. Gration Kamugisha
(kushoto) mara baada ya kumaliza zoezi la wakiweka sahihi mikataba ya
makubaliano ya uendelezaji wa maeneo hayo yanayomilikiwa na wizara
katika balozi mbalimbali ili yawe na manufaa kibiashara huku
wakishuudiwa na wasaidizi wao.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula (kulia)
wakipeana mikono na na mtendaji mkuu wa UTT-PID Dr. Gration Kamugisha
(kushoto) mara baada ya kumaliza zoezi la wakiweka sahihi mikataba ya
makubaliano ya uendelezaji wa maeneo hayo yanayomilikiwa na wizara
katika balozi mbalimbali ili yawe na manufaa kibiashara huku
wakishuudiwa na wasaidizi wao.
Picha ya pamoja ya watumishi wa UTT-PID pamoja na Balozi Liberata Mulamula baada ya kutia sahihi Makubaliano hayo.
Katika
makubaliano hayo UTT-PID kwa kutumia mitaji itakayopatikana kupitia
vyanzo mbalimbali ikiwemo Hati Fungani, Miundombinu ya aina tofauti
ikiwemo majengo ya biashara na ofisi za kisasa za Ubalozi itawekezwa
katika maeneo hayo ya balozi zetu katika mataifa mbalimbali ili iweze
kuwa moja ya vyanzo vya mapato vya Serikali ya Tanzania kupitia tozo za
kodi zitakazopatikana kutoka kwa wapangaji wa kada tofauti katika
uwekezaji huo.
Pia
itapunguza gharama za uendeshaji wa balozi zetu na hata kwa nchi ambazo
Serikali imelazimu kupanga kwa ajili ya ofisi za Ubalozi ikijumuisha
kuokoa fedha nyingi zitokanazo na ulipaji wa kodi ya pango. Akitolea
mfano Katibu Mkuu Balozi Mulamula alisema kuna nchi ambazo wizara
inalazimu kulipa kati ya USD 10,000 mpaka 15,000 kwa mwaka kwa ajili tu
ya Pango la ubalozi.
Kwa
hiyo kwa uwekezaji kama huu siku za usoni Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa itaokoa fedha nyingi ya bajeti ambayo inatumika
kulipia pango hususani katika nchi ambazo hakuna majengo ya ubalozi
yanayomilikiwa na Wizara.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni