Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi leo
amefunga kozi ya waamuzi chipukizi wasiokuwa na beji za FIFA katika
hoteli ya Holiday, ambapo jumla ya waamuzi 30 kutoka nchi 28 barani
Afrika walihudhuria.
Akiongea wakati wa kufunga kozi hiyo
Malinzi alitoa wito kwa wahitimu wajikite kwenye maadili kwa kuzingatia
mafunzo waliyopata ili katika kipindi kifupi wote wapate beji za FIFA na
waonekane kweye mashindano makubwa kama fainali za AFCON na mashindano
ya Kombe la Dunia.
Kabla ya Hotuba ya Mgeni rasmi mwakilishi wa
CAF Eddy aliishukuru TFF kwa maandalizi mazuri na usimamizi bora kwa
kipindi chore cha kozi hii, na kuahidi kuleta kozi nyingine kubwa hapa
nchini.
Naye mwakilishi wa FIFA Carlos Hendrique alitoa
shukurani zake za dhati kwa TFF kwa kuwa tayari wakati wote kushirikiana
na FIFA hali ambayo imefanyika TFF iaminike na itegemewe na FIFA kweye
program mbalimbali
Kozi hiyo ya waamuzi imefanyika kwa mara ya kwanza hapa barani Afrika.
FIFA
iliiteua Tanzania kuwa mwenyeji wa kozi hii kwa nchi zinazo zungumza
kiingereza. Kwa upande wa nchi zinazo zungumza kifaransa kozi ya aina
hii imefanyika nchini Morocco
Washiriki 30 kutoka nchi 28
barani Afrika wamehudhuria kozi hii ilivyokuwa itafundishwa na Wakufunzi
wa Sita kutoka CAF na FIFA.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni