Rais
Kikwete anatarajia kuzindua Kituo Kituo cha Michezo cha Kisasa cha
Jakaya M. Kikwete Youth Park (JMK Park), Kidongo Chekundu, Dar es
Salaam, kituo cha kwanza cha aina yake nchini chenye kulenga miongoni
mwa mambo mengi kuanza kulea wanamichezo tokea wakiwa wadogo.
Hayo yalijitokeza wakati wa mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Umeme ya Symbion Power, Bwana Paul Hinks(pichani) kwenye Hoteli ya JW Marriot Essex House, mjini New York, Marekani ambako Rais alikuwa anafanya ziara rasmi ya kikazi. Rais Kikwete alikiwekea Kituo hicho jiwe la msingi mwaka jana.
Katika
mkutano huo, uliofanyika jana, Jumanne, Septemba 29, 2015, Bwana Hinks
alimweleza Rais Kikwete kuwa ujenzi wa Kituo hicho sasa umekamilika
tayari kwa uzinduzi na hivyo kuongeza thamani kubwa kwenye eneo ambalo
miaka ya nyuma lilikuwa gereji ya kutengenezea magari.
Kituo
hicho cha JMK Park kimegharimu kiasi cha dola za Marekani milioni mbili
na ni matokeo ya ushirikiano ya Kampuni ya Symbion Power ya Marekani,
Klabu ya Soka la Ligi Kuu ya Uingereza ya Sunderland AFC na Taasisi ya
Grasshopper Soccer. (Picha na Freddy Maro).
Hayo yalijitokeza wakati wa mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Umeme ya Symbion Power, Bwana Paul Hinks(pichani) kwenye Hoteli ya JW Marriot Essex House, mjini New York, Marekani ambako Rais alikuwa anafanya ziara rasmi ya kikazi. Rais Kikwete alikiwekea Kituo hicho jiwe la msingi mwaka jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni