BALOZI SEFUE AWASISITIZA WATUMISHI WA UMMA KUVAA BEJI ZENYE MAJINA YAO WANAPOKUWA KATIKA MAENEO YAO YA KAZI
posted on
“Nimeamua kuonyesha mfano kwa vitendo kufuatia agizo nililolitoa kwa watumishi wa Umma kwa kuvaa beji inayonitambulisha jina langu , nilisema nitakuwa wa kwanza kuvaa jina langu nimevaa. Kama mtumishi wa umma atakuwa na mashaka ajue mimi nimeshalivaa”.
“Mtumishi wa umma anapomuhudumia mwananchi ni lazima ajue amehudumiwa na nani, mtumishi wa Umma akifanya kazi zake kwa kutenda haki sidhani kama ataogopa kuvaa beji inayomtambulisha jina lake hivyo basi kama nilivyoagiza watumishi wote wa Umma mvae beji zinazowatambulisha majina yenu”, alisisitiza Mhe. Balozi Sefue.
Mhe. Balozi Sefue alifanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO) dhidi ya Standard Bank.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni