Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo nchini, Mhe. Juma – Alfani Mpango ambaye alikwenda ofisini
kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago Balozi wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Mhe. Juma-Alfani Mpango ambaye
alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015
kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo, Mhe. Juma- Alfani Mpango ambaye alikwenda ofisini kwa
Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambaye anamaliza muda wake, Bw.
Juma-Alfani Mpango.
Akizungumza na balozi Mpango leo
(Jumatano, Desemba 2, 2015), ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es
Salaam, Waziri Mkuu alimshukuru balozi huyo kwa pongezi zake na kumuomba
aendelee kuwa balozi mzuri wa kuitangaza Tanzania hata baada ya kurejea
nyumbani.
Pia alitumia fursa hiyo kuwaombea heri wananchi wa
DRC pamoja na Rais Joseph Kabila katika maandalizi ya uchaguzi mkuu
ambao unatarajiwa kufanyika nchini humo mwakani.
Kwa upande wake, Balozi Mpango ambaye alisema amekaa hapa nchini kwa
miaka 12, alimweleza Waziri Mkuu kwamba amejifunza mengi sana kutoka kwa
viongozi wa Tanzania kubwa vikiwa ni uchapakazi na unyenyekevu.
“Nimeona utawala wa Rais Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete na sasa
Dkt. John Pombe Magufuli. Ninavutiwa na hatua mnazochukua hivi sasa
katika kupambana na rushwa na ufisadi,” alisema.
“Mambo
niliyojifunza tangu nimekaa hapa ni uchapakazi na unyenyekevu. Unaona
kabisa kwamba mtu anaamini kuwa madaraka siyo kitu cha kujivunia kwa
mtumishi wa umma. Anachotakiwa kuwa nacho ni utayari wa kuwatumikia
wananchi,” alisema kwa Kiswahili sanifu.
Balozi Mpango aliomba
mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe kwani DRC imekuwa ikinufaika
na matumizi ya bandari ya Dar es Salaam katika kusafirishia bidhaa zake
kwenda nchi za nje.
“Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu sana
kwetu. Mwaka 2004 tulisafirisha tani za mizigo 200,000, mwaka 2014
ziliongezeka na kufikia tani milioni 1.3; na mwakani tunataraji
zitaongezeka na kufikia tani milioni tatu,” alisema.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni