Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda (kulia), akizungumza na Watendaji na Viongozi wa Serikali za
Mitaa wa wilaya hiyo kwenye mkutano uliofanyika Dar es Salaam leo kuhusu
jinsi ya kutatua na kukomesha kero za ardhi
Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Makonda (hayupo pichani)
Na Dotto Mwaibale
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ametoa siku
20 kwa Wenyeviti wote wa Serikali za Mitaa Manispaa hiyo kuwa na ramani
ya mitaa ili kuyatambua maeneo ya wazi.
Makonda amewataka watendaji wa Manispaa
hiyo kwenda na kasi ya serikali ya kuwatendea haki wananchi katika
kumaliza migogoro ya ardhi.
Akizungumza Dar es Salaam leo mchana na
Wenyeviti zaidi ya 100 wa Serikali za Mitaa ya9 Manispaa ya Kinondoni
,Makonda alisema baadhi ya watendaji wanatanguliza maslahi mbele kuliko
mahitaji ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Alisema migogoro ya ardhi ni kero kila
sehemu misibani, harusini na kwenye mazishi suala kubwa ni la ardhi na
kuongeza kuwa mabaraza ya ardhi ya Kata hayana uhalali wa kuamua kesi
hizo kwa kuwa baadhi yao hata uelewa wa masuala hayo hawana na yamekuwa
yakiongeza matatizo.
"Leo tumekutana hapa kwa sababu ya
migogoro ya ardhi na kuanzia sasa ndani ya Wilaya ya Kinondoni nataka
kurudisha heshima ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa nawaagiza kuanzia
sasa mtu yeyote kutoka Wizarani,Manispaa au hata mwekezaji lazima apitie
kwanza kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa,"alisema.
Alisema watendaji wengi Manispaa ndio
chanzo cha migogoro ya ardhi kwa kutotimiza wajibu wao na wameshindwa
kuonyesha dira ya kuwasaidia wananchi.
"Kibaya zaidi ili kujitengenezea
mazingira ya ulaji wenyeviti hawashirikishwi katika hatua za awali
wanahusika zaidi pale kunapotokea mgogoro,"alisema.
Aliongeza kuwa "Sina hofu wala uoga wala
sina sifa ya kupendwa wala kutafuta kupendwa hivyo nitahakikisha
ninatumia Mamlaka niliyopewa kufanya migogoro hii ya ardhi Kinondoni na
kuwa historia na nikitaka jambo huwa sishindwi"alisema.
Alisema baada ya wenyeviti hao kupewa
ramani atahakikisha anakutana na Wazi ri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Wilium Lukuvi na maofisa wa ardhi.
"Hapo sasa watakaobainika kuhusika
katika michezo michafu na kuchochea migogoro basi Waziri Lukuvi aondoke
nao maana wameshindwa kazi"alisema
Makonda aliwataka wenyeviti hao kuonesha
maeneo ya wazi na yale yaliyovamiwa ili kuchukua hatua kwani wenye
dhamana wapo ofisini huku wananchi wakiwa wanateseka na migogoro hiyo.
Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Manispaa
ya Kinondoni Juliana Letara alisema Wenyeviti wote watapewa ramani za
mitaa yao ndani ya wiki mbili kwa kuwa zipo kwenye kompyuta ofisini
hivyo atawapatia ramani hizo.
Alisema kutokana na migogoro mingi ya
ardhi anapendekeza kufanyike mapendekezo ya mabadiliko ya sheria kwa
kuwa kesi zote za mabaraza ya kata zinaigharimu serikali zaidi ya
milioni tatu kwa siku.
Alizitaja kesi hizo kuwa ni za ardhi ya hifadhi,ardhi ya kawaida na ile ya kimila
"Tulikopa benki ya TIB mkopo kwa ajili
ya kupima Viwanja likiwemo eneo la Mabwepande lakini kila siku tunatozwa
riba ya sh.milioni tatu jambo ambalo ni gumu na ipo siku litashindikana
na ndio maana tunauza Kiwanja hadi milioni 20 na 30,"alisema.
Baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa
ambao walipata nafasi ya kuzungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo
walimtaka Makonda kuondoa majipu sugu katika Manispaa hiyo likiwemo la
maofisa mipango miji.
Alisema wako tayari kufanyazi na
Makonda lakini sio wafanyakazi hao kitengo cha ardhi kwa kuwa wamekuwa
chanzo cha migogoro mikubwa ya ardhi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni