Na. Ahmad Mmow,Nachingwea.
Baadhi
ya madiwani na wafanyabiashara wa mazao ya misitu Wilayani Nachingwea
mkoani Lindi, wamelalamikia urasimu wa utoaji wa vibali vya kusafirishia
mazao ya misitu, unaofanywa na wakala wa huduma za misitu(TFS)
unaosababisha wafanyabisha wa mazao ya misitu kukwepa kwenda vijijini
kununua na kuvuna mazao ya misitu.
Madiwani
na wafanyabiashara hao, waliyasema hayo kwenye kikao cha mrejesho wa
mchakato wa uwajibikaji wa jamii katika usimamizi wa misitu,
kilichoendeshwa na kuandaliwa na shirika lisilo la kiserika la jukwaa la
sera (Policy forum) kwa ufadhili wa kampeni ya mama misitu,
kilichofanyika jana, mjini Nachingwea.
Walisema
kumekuwa na urasimu mkubwa unaofanya na wakala huduma za misitu katika
utoaji wa vibali vya kusafirishia kwa wafanyabiashara. Hali
inayosababisha wafanyabiashara kukwepa kwenda vijijini kununua na kuvuna
mazao ya misitu na kusababisha soko la mazao kuwa gumu.
Mfanyabiashara,
Polycap Cassian alisema kutokana na urasimu uliopo wakupata vibali vya
kusafirishia, wafanyabiashara wanaogopa kwenda vijijini kuvuna na
kununua mazao ya misitu. Hivyo wananchi ambao walikuwa na matarajio ya
kunufaika na misitu wanakata tamaa.
Alisema
kuna mzunguko mrefu wa kupata vibali vya kusafirishia, ambao
unasababisha wapoteze muda mwingi wa kufanyabiashara. Hivyo alishauri
vijiji vipewe uwezo wa kutoa vibali vya kusafirishia.
Diwani wa kata ya Mkotokuyana, Sada Makota, licha ya kulaumu urasimu katika utoaji wa vibali hivyo, lakini pia alilaumu mamlaka hiyo kugonga na kuweka alama zinazoruhusu kusafirishwa mbao zilizopasuliwa kwa kutumia misumeno ya moto(chain saw).
"Ingawa
halmashauri imewaagiza maofisa wake wa idara ya maliasili kutogonga
mbao zilichanwa kwa chenisoo lakini wenzetu wanazigonga na kuziruhusu
zisafirishwe,"alisema Saada.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Ahmad Makoroganya, alisema
ingawa wamekuwa wakitoa maagizo kwa maofisa waliochini ya halmashauri
kutozigonga mbao zilizopasuliwa kwa misumeno hiyo, lakini imekuwa ni
vigumu kudhibiti uvunaji unaotumia mashine ya hizo.
Kwamadai
kuwa maagizo hayo yanaishia na kutekelezwa na maofisa hao waliochini
halmashauri, wakati maofisa wa wakala huduma za misitu wazigonga na
kuzipitisha.
Alisema hakukuwa na sababu ya wilaya kuwa na mameneja wa wakala wa misitu wakati kunamaofisa wa misitu wa wilaya.
"wakati
misitu ipo ndani ya vijiji, wanatuletea meneja wasio wajibika kwetu"
turejeshewe mamlaka kamili kwenye misitu, maana kunakitu hapa pembeni
kinatuangusha,"alisisitiza Makoroganya.
Ofisa
misitu wa Wilaya ya Nachingwea, Paiton Kamnana, alisema ingawa sheria
inasema ofisi za idara za misitu inaweza kutoa vibali hivyo, lakini
utekelezaji wake bado kufanyika na wizara ya maliasili na utalii.
Alishauri
kuwepo mawasiliano ya mara kwa mara baina ya Halmashauri ya Wilaya na
ofisi ya kanda ya wakala wa huduma za misitu kwani dhamira na malengo ni
ya aina moja ambayo ni kuona jamii na taifa linanufaika na maliasili
zilizopo nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni