Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akiongeawakati wa tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akielekea katika boma la mbwa mwitu kwa ajili ya tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akikata utepe kuruhusu kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kutoka nje kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
Wanahabari wakichukua picha mbalimbali wakati mbwa mwitu walipokuwa wakitoka kwenye boma.Kundi la sita la mbwa mwitu 11 wakitoka katika boma maalum katika Hifadhi ya Serengeti.Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi akiongea na wanahabari mara baada ya tukio la kuachiwa kwa mbwa mwitu.Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (MB) akiwa katika picha ya pamoja na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (MB) akisalimiana na Mhifadhi Ashery Loishooki mara baada ya kuwasili katika eneo la Nyasirori, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita katika boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi (aliyesimama) akitoa neno la ukaribisho kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) katika tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu
.………………………………………………
Waziri
wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amepongeza jitihada
zinazofanywa na watafiti kwa kurudisha mbwa mwitu katika Hifadhi ya
Taifa Serengeti baada ya kutoweka katika miaka ya tisini. Waziri
Maghembe alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki alipokuwa akiachia huru
kundi la sita la mbwa 17 waliokuwa wamehifadhiwa katika boma maalum ili
kurejea katika makazi yao ya asili.
Profesa Maghembe amesema serikali itaendelea kuwekeza katika eneo la utafiti ili kuwezesha sekta ya uhifadhi nchini kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa. Alisema mabadiliko ya tabia nchi yameathiri sekta nyingi ikiwemo ya uhifadhi na kuwa wanyama wamekuwa wakiathirika na mabadiliko hayo hivyo ni vema uwekezaji mkubwa ukafanyika katika eneo la utafiti ili kujua namna ambavyo uhifadhi unaweza kukabiliana na mabadiliko hayo.
Mradi wa uhifadhi wa mbwa mwitu unalenga kurudisha mbwa mwitu katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambao walitoweka kabisa tangu mwaka 1994 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaweza kubainika kisayansi. Mradi huu unasimamiwa na kuendeshwa na watafiti wa kitanzania.
Tangu kuanza kwa mradi huu mwaka 2011, jumla ya makundi sita ya mbwa mwitu wamesharudishwa ndani ya Hifadhi ya Serengeti. Makundi haya ni pamoja na Vodacom ambapo Kampuni hii ya simu ilifadhili gharama za mradi; Serengeti; Loliondo; Kikwete; Nyasirori na hili la mwisho ambalo lilipewa jina la Markus Borner, mwanasayansi kutoka nchini Ujerumani aliyetumia miaka 35 akifanya shughuli za uhifadhi katika hifadhi ya Serengeti.
Mradi wa mbwa mwitu Serengeti unaendeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, TANAPA na Chuo Kikuu cha Glasgow.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni