Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akikabidhi hundi kwa Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Msalala Patrick Karangwa,ikishuhudiwa na Mkuu wa
wilaya ya Kahama Vita Kawawa(katikati)
Baadhi
ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mgodi wa Bulyanhulu
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Vita Kawawa akizungumza wakati wa ziara yake katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ambapo amesisitiza
kuwa kodi ya ushuru wa huduma iliyotolewa na Mgodi wa Bulyanhulu
itumike vizuri kujenga miundombinu ambayo wananchi wataiona kwa macho
Afisa
Maendeleo na Mahusiano wa mgodi wa Bulyahulu ,Sara Teri akisalimiana na
Mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa,kushoto kwake ni Mshauri wa
Mahusiano ya Kampuni ya Acacia na Serikali , Alex Lugendo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa (Kushoto) akielekea katika eneo la mgodi wa chini ya ardhi Bulyanhulu.
Mkuu
wa wilaya ya kahama Vita Kawawa na ujumbe wake pamoja na mshauri wa
mahusiano ya kampuni na serikali wa Acacia aliyesimama katikati mwenye
shati ya bluu Alex Lugendo wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa Akiwa chini ya archi kilomita moja
kutoka uso wa dunia akiwapongeza wafanyakazi wazawa katika mgodi wa
Bulyanhulu kwa kufanya kazi ambazo zamani watanzania walikuwa hawawezi,
kazi ya kufanya kazi kwa mitambo ya kisasa ya inayojulikana kama Jumbo
na mashine zingine za teknolojia ya kisasa zinazotumika katika kuchimba
dhahabu kwenye mgodi mkubwa wa dhahabu nchini Bulyanhulu.
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa Akiwa anatoka kwenye lifti kutokea
chini ya ardhi baada ya kutembelea mgodi wa dhahabu chini ya ardhi.
Kaimu Meneja wa Uchimbaji katika Mgodi wa Bulyanhulu Salvatory Tesha
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Bw.Graham Crew akifafanua jambo kwa mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa.
Meneja
wa Ufanisi wa Kampuni katika Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Elias
Kasitila akimuonyesha ramani ya uchimbaji mkuu wa Wilaya ya Kahama na
ujumbe wake
Na Dixon Busagaga wa Globu
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama Mhe. Vita Kawawa amemwagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Msalala kuwa fedha zitumike vizuri katika miradi
inayoonekana.
“sitaki
masuala ya kusema unajua pesa tuliitumia katika kuweka kifusi
barabarani na sasa mvua imekiosha, hapana, hilo litakuwa ni jipu
linatakiwa kutumbuliwa, fedha hizi zitumike kujenga miradi inayoonekana
kama vila vyumba vya madarasa, zahanati nakadhalika.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni