Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana
na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik wakati alipowasili
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee tayari kwa kuongea na wazee wa mkoa wa
Dar es salaam jana ambapo mkutano huo pia ulihudhuriwa na Makamu wa Rais
Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amehudhuria katika
mkutano huo ambapo alionekana mtu mwenye kufurahia hotuba hiyo.
Mwanzoni
Askofu Gwajima alipofika ukumbini hapo alikuta ratiba inaendelea
hivyo ilibidi akae viti vya nyuma lakini Shekh Mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim alimpigia simu na kumwomba aende mbele
akakae pamoja na viongozi wenzake wa dini.
(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Msafara
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli
ukiwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jana wakati alipoongea na
wazee wa mkoa wa Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana
na Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa wa Dar es salaam mzee Hemed Mkali kutoka
kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Raymond Mushi na Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana
na Mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es salaam wa zamani Mzee Idd
Simba, Kulia ni mfanyabiashara Abdullah Mohamed.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza
na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Majaliwa Kassim
Majaliwa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, Makamu wa
Rais Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim
Majaliwa na Mke wa Rais Mama Janet Magufuli wakiwa meza kuu pamoja na
viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam.
Baadhi ya mawaziri wa wizara mbalimbali katika serikali ya awamu ya tano wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo na ya Kiislamu wanaounda kamati ya Amani wakiwa katika mkutano huo
Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima hakubaki nyuma na yeye
amehudhuria katika mkutano huo na hapa akionekana mwenye furaha na
bashasha kama alivyonaswa na kamera yetu.
Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa amekaa pamoja na
viongozi wenzake wa dini katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
salaam wakati Rais Dk. John Pombe Magufuli alipozungumza na wazee wa
mkoa wa Dar es salaam.
Baadhi ya wazee wa Dar es salaam wakitambulishwa katika mkutano huo.
Baadhi
ya mawaziri waliohudhuria katika mkutano huo kutoka kulia ni Mh.
Profesa Sospeter Muhongo, Dk. Abdallah Posi, Nape Nnauye, Januari
Makamba na Ummy Mwalimu.
Baadhi
ya wazee wakifuatilia kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia mkutano huo.
Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akisalimia wazee katika mkutano huo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimia wazee katika mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Wazee wa mkoa wa Dar es alaam Mzee Hemed Mkali akihutubia katika
mkutano huo na kumkaribisha Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kuwahutubia
wazee hao.
Wazee hawa wakionekana kuhamasika na hotuba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni