Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Rais
Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa
ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi
walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias
Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau.
Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.
Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:
1.
Naibu
Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa
Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya
Dar es salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa wazi na
Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.
2. Naibu
Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa
Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na
Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa wazi na
Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
3. Naibu
Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa
Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya
Intelijensia.Kamishna Mikomangwa anajaza
nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU).
4. Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Nsato Marijani Mssanzya ambaye
amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara
ya Mafunzo na Operesheni. Kamishna Mssanzya anajaza nafasi iliyoachwa
wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya
Udhibiti (Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya
Tanzania. Dkt. Kipilimba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson
Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Teuzi zote zinaanzia leo tarehe 15 Februari, 2016
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni