Marehemu Michael Denis a.k.a Joni Woka enzi za uhai wake
Akiongea kwa simu kaka wa marehemu Omari Milay, amesema walipigiwa simu alfajiri ya jana na kujulishwa kuwa Michael Denis aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa jina la Joni Woka amefariki katika hospitali ya Muhimbili, alipokuwa akipata matibabu ya ajali aliyopata siku ya jana.

Michael Denis a.k.a Joni Woka alipata ajali ya kugongwa na kitu kizito kwenye paji la uso, alipokuwa gereji maeneo ya Sinza akitengeneza gari yake, kwa bahati mbaya mtungi wa gesi ukalipuka na moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani.
Tarifa za awali za madaktari zilisema wanahofia kipande hiko kimefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.
Mipango ya mazishi familia imesema inakutana kujadili na mara itakapokamilika watajulisha watu nini kinaendelea.
Msanii John Woka ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family, alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za Sophia, baby gal na nyinginezo, ambazo aliziimba kwa mtindo wa ulevi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni