Bw Polepole akimpongeza mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela wakati wa kongamano la shirikisho la vyuo vya elimu ya juu la wana CCM mkoa wa Iringa jana |
.Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela akiwa amembeba mmoja
kati ya watoto wakazi wa kijiji cha Mboliboli tarafa ya Pawaga wilaya
ya Iringa ambao wamekumbwa na mafuriko ambayo maji yake yana vimelea
vya ugonjwa wa kipindupindu kwa zaidi ya siku nne sasa baadhi yao
bado wanaishi juu ya vichuguu
Mkuu wa wilaya ya Iringa akizungunza na wananchi waliookolewa katika mafuriko Pawaga
Mkuu
wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela akizungumza na wanafuzi wa
vyuo vikuu mkoa wa Iringa wakati wa kongamano la jana kushoto ni Bw
Polepole na kulia na kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Bw salim Asas na
katibu wa shirikisho hilo Bi mariam Fundi
Na MatukiodaimaBlog
ALIYEKUWA
mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba BW Humphrey Pole pole
amempongeza mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela kwa kazi
kubwa na nzuri anayoifanya ya kujitoa kunusuru uhai wa wananchi wa
kata ya Mboliboli tarafa ya Pawaga ambao wamekubwa na mafuriko yenye
vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu kuwa mkuu huyo wa wilaya ni
hazina kubwa ya Taifa na kumwomba Rais Dr John Magufuli kumkumbuka
katika ufalme wake.
Huku
akidai kuwa kazi inayoendelea kufanywa na rais Dr Magufuli ya
kutumbua majipu wapo ambao wanaumizwa zaidi kutokana na kupoteza imani
ya kuendelea kuishi maisha ya kula bata kila uchwao.
Bw
Polepole ambae alikuwa ni mgeni rasmi katika kongamano la miaka 39 ya
kuzaliwa kwa CCM na siku 100 za Rais Dr Magufuli lililoandaliwa na
shirikisho la vyuo vya elimu ya juu la chama cha Mapinduzi (CCM)
mkoani Iringa lililofanyika jana mjini hapa alisema kuwa amepata
kushuhudia kupitia vyombo vya habari mbali mbali jinsi ambavyo mkuu
huyo wa wilaya ya Iringa Bw Kasesela anavyojitolea kuokoa maisha ya
wananchi wake jambo ambalo kwa viongozi wengine ni vigumu kufanya
hivyo.
Alisema
kuwa kati ya wakuu wa wilaya ambao wamekuwa wakiitambua kazi yao kwa
wananchi na wananchi wakiona bila tatizo kazi inayofanywa na kiongozi
wao ni pamoja na mkuu huyo wa wilaya ya Iringa ambae ushujaa na
uzalendo wake kwa wananchi wake ni mkubwa na mfano wa kuigwa na
viongozi wengine katika kuwatumikia wananchi.
"
Tanzania ya Rais Dr Magufuli itapiga hatua kubwa zaidi ya leo
tunapotathimini siku 100 za utawala wake iwapo watendaji wote
watatambua wajibu wao kwa wananchi wao badala ya kutangulia maslahi
yao kwa taifa yao....nimependezwa sana na moyo wa kujitolea kwa
ajili ya wananchi ambao mkuu huyu wa wilaya kakangu Richard Kasesela
anaonyesha ni mmoja kati ya wakuu wa wilaya ambao wanafanya kazi kwa
moyo .....nimeona katika mitandao ya kijamii mkuu huyu wa wilaya
akiogelea katika maji kuokoa maisha ya wananchi wake ambao wamekubwa na
mafuriko tena maji yenye vimelea vya kipindupindu ....ni nani angeweza
kuhatarisha maisha yake hivi zaidi ya kutuma waliopo chini yake
kufanya kazi kwa niaba yake" alihoji Bw polepole.
Huku
akimtaka mkuu huyo wa wilaya kuzidi kutumika vema kwa ajili ya
wananchi wake na kuomba iwapo inawezekana Rais Dr Magufuli kwenye
utumbuaji wake wa majipu kwa wakuu wa wilaya na mikoa kuangalia
wakuu wa wilaya wasio tambua wajibu wao ambao wapo kwa ajili ya faida
yao na kuwaacha ama kuwapandisha vyeo zaidi wale ambao wamekuwa
wakifanya vizuri.
"
Simpigii debe Kasesela ila naongea ukweli ulio wazi kwa kila mmoja
wenu hasa watu wa Iringa ambao mmekuwa nae ....binafsi nimevutiwa na
utendaji wake mzuri nampongeza sana".
Hata
hivyo Bw Polepole alisema kuwa kazi inayofanywa na Rais Dr Magufuli
ya kutumbua majipu ni kazi ya nzuri kwa watanzania swapenda uzalendo
ila wapo wanaoumia kwa ndugu zao ama wenyewe kutokuwa na uhakika wa
kuendelea kufanya anasa za matumizi ya pesa ama kupata mkate wa kila
siku.
"
Hii ni kazi nzuri sana na inapaswa kuendelea kwa nguvu zote ...ila
tuwe wakweli hapa wengi tunashangilia kuona majipu ambayo si ndugu
yanatumbuliwa hivi inakuwaje kama zamu ya kutumbua jipu ingekuhusu wewe
ama mzazi wako .....bila shaka ungeona zoezi hili ni baya zaidi
lakini kwa ajili ya kuifanya Tanzania kuwa ya wote lazima tuwe
wapole tuache kila jipu litumbuliwe kwa afya yako ".
Aidha
alisema utendaji mzuri wa Dr Magufuli na serikali yake ya CCM
umepelekea wapinzani nchini kukosa hoja ya kuzungumza na kuendelea
kuokoteza maneno ya kuongea ili mradi waonekane wameongea jambo lakini
kimoyo moyo wanapongeza kazi nzuri ya serikali ya CCM chini ya rais
Dr Magufuli.
Pia
alipongeza imani kubwa ya wanachama wa chama cha Demokrasia na
maendeleo (Chadema) kutoka vyuo vikuu vya Iringa ambao wamehama
vyama hivyo na kujiunga na CCM baada ya kupendezwa na utendaji mzuri
wa Rais Dr Magufuli katika kutekeleza Ilani ya CCM na kuwataka
wengine kuzidi kurudi CCM kwani wapende wasipende kasi ya rais Dr
Magufuli ni kubwa tofauti na walivyotegemea.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Bw kasesela pamoja na
kumpongeza Bw polepole kwa kuendelea kuelimisha umma kupitia vyombo
mbali mbali vya habari juu sera nzuri za CCM na kutambua kazi
anayoifanya yeye kama mkuu wa wilaya ,bado alitaka wasomi nchini
kutokubali kupandikizwa siasa chafu za kulalamika na kutuhumu kila
uchwao na badala yake wao kuwa msaada kwa umma.
Alisema
wapo baadhi ya wana siasa wanatumia wasomi kuhadaha umma kwa faida
yao badala ya kuelimisha umma kwa kueleza ukweli nini CCM imefanya
kwa miaka yake 39.
"
wapo baadhi ya wanasiasa wao kazi kwao ni kusema ovyo ovyo serikali
ya CCM na wengine wapo hadi Iringa ambao wao bila kutukana ama
kuisema vibaya serikali ya CCM kwao siku haijapita .... binafsi
sitanyamaza kuona mwana siasa ama mtu yeyote akimsema ovyoovyo Rais
wangu Dr John Pombe Magufuli kama akiongea mbele yangu ngumi moja
mbili nitampa na akiongeza mbali ya mimi kama katika vyombo vya habari
nitamjibu haraka.....siwezi hata siku moja kuvumilia mtu msema ovyo
heri hata huu ukuu wa wilaya nipoteze kwa kuitetea serikali yangu ya
CCM"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni